Wazungu Weusi
Watu kama wewe, wajinga na wasiojiheshimu ni ninyi mnaouza ardhi yetu kwa Wazungu. Ninyi m’Wazungu weusi na ninyi ndio adui wakubwa wa Waafrika. Ni ninyi mnaozuia uhuru wetu. Na ninyi lazima muangamizwe.
Askari wake waliomlinda Chifu po pote alipokwenda, walianza kuonyesha hasira walipoona kwamba Mumbi hakumjibu Chifu. Maina, mmoja wao, alianza kushikashika kiboko cha ngozi ya kifaru, alichokichukua kila mahali walipokwenda. Chifu na askari wake walikitumia kiboko hiki kwa kuwapiga wale watu walioshtakiwa kuwa ni wafuasi wa Mau Mau.
Waliposhuka chini, Chifu aliwapiga risasi na kuwauwa papo hapo. Huko kijijini, aliwaambia watu kwamba Maciira na wenzake walikuwa wakijaribu kutoroka kuelekea msituni kwa hivyo askari wakalazimika kuwapiga risasi na kuwauwa. Hakuna mtu aliyethubutu kutokubaliana na habari hii, kwani angefanya hivyo, yeye vile vile angefanyiwa kama wao.
Askari wote walijiona wamevalia vizuri sana. Hii ilikuwa ni kweli kwa sababu watu wengine wote walikuwa wachafu and wamerarukiwa na nguo zao sana. Watu wote, waume, wake na watoto, walikuwa ni lazima kukaa vijijini mwao bila kutoka nje.
Huko vijijini, wake hawa walipewa jina la “Wake wa Hali ya Hatari”. Wengine ambao hawakuolewa, walipewa jina la “Rarua” kwa vile walizoea kurarua chapati nyumbani mwa askari.
Kwa sababu hii mpango ulifanywa, na viongozi wengine wakatumwa mpaka Ngaini jioni moja kwenda kumchukua Mzee na kumpeleka pale sherehe ilipokuwa imetayarishwa. Shauri lilikuwa limekatwa kuwa, kama akikataa kula kiapo, na ilifikiriwa hangekataa, angenyakuliwa na kupelekwa msituni auawe.
Mau Mau
Yule kijana alikuwa ameshtakiwa sio tu kwa kula kiapo lakini vile vile kwa kulisha kiapo na kuchukua bunduki. Haya yalikuwa mashtaka mabaya sana, maana yeyote aliyeshtakiwa na kuhukumiwa kwa makosa kama hayo, alikuwa ni lazima kunyongwa au kufungwa jela zaidi ya miaka kumi.
Vijana askari wa Kiafrika, walipigana na kupoteza maisha yao wakitumaini kwamba vita vikiisha na wao wakirudi nyumbani kwao, serikali itawaheshimu na hapatakuwako na ubaguzi hotelini, barabarani au kazini. Walifikiri watapewa mshahara sawa na Wazungu ikiwa walikuwa na ujuzi sawa sawa. Vile vile walitumaini kwamba wale wasio na mashamba watapatiwa.
Walikasirika zaidi walipokumbuka siku moja huko Colombo, baada ya kuwazika askari wa Kiafrika waliouliwa huko Burma, vile Kapteni wao alipowaambia kwamba, kwa kzai nzuri Waafrika waliyoifanyia serikali ya Mfalme, watasaidiwa na kuheshimiwa wairudi kwao Kenya. Lakini waliporudi, hawakupata msaada wowote. Wale waliopata msaada ni vijana Wazungu, ambao ndio walipatiwa mashamba huko upande was Naromoru na kwengineko.
Meja Blue na rafikiye walisafiri kuelekea Kiganjo, na huko njiani walifurahi kuona vile jua la jioni lilivyokuwa limeifanya nchi nzima kuwa nzuri. Meja Blue hakutafuta kazi. Alichaguliwa kuingia msituni kama askari wa Mau Mau.
Alipewa uhuru was kuwatambulisha wale watu ambao walikuwa wamekula kiapo na baadaye wakakataa kuwasaidia Mau Mau kama walivyoahidi. Serikali ilimfikiria kuwa mtu mzuri sana na hakuna wakati wowote ilipomfikiria kuwa mshiriki wa Mau Mau.
Rafiki wa Mau Mau
Moyoni alijua hakuwa na lolote la kufanya, ila alijua kwamba hata kama akisema amekula au hajala kiapo, ilikuwa sawa tu. Alikumbuka rafiki yake Nyaguthii. Yeye alikubali kwamba alikuwa amekula viapo viwili. Aliwataja wote waliomlisha na wale waliokula pamoja naye. Lakini hata hivyo, alihukumiwa na kutiwa korokoroni huko Kamiti kwa muda wa miaka minne. Alopkuwa huko alipigwa na askari wa jela mpaka akafa, lakini watu wa jela wakasema alikufa baada kuugua.
Sio tu wakaaji wa mtaa huo, lakini hata na wakaaji wa mashamba yaliyozunguka Kiganjo walifika hapo usiku huo na kula hicho kiapo. Asubuhi wote walirudi kila mtu mahali alipofanya kazi na hakuna aliyesema lile lililofanyika usiku ule.
Walipofika hapo Ragati, saa za usiku madereva hao walizitupa chini, na pale zikaokotwa na wasaidizi wa Mau Mau, hasa wanawake, walioishi hapo kama raia wema wa Serikali. Walizipitisha kwa siri mpaka zikawafikia askari wa Mau Mau huko msituni.
Ukiwa mwalimu au mtu yeyote ambaye ameajiriwa waweza kusaidia kwa pesa. Ukiwa mkulima waweza kusaidia kwa chakula. Ukiwa huna chochote, waweza kusaidia kwa kupasha habari.
Maisha ya Wananchi
Kwa vile watu hawakukubaliwa kulima, mashamba yao kwa mwezi mzima, majani mengi yalikuwa yamemea na kulifanya shamba liwe kama kichaka.
WAHU. Utarudi lini ama utanisahau ukienda Nairobi?
MEJA BLUE. La,
sitakusahau. Nikipata kazi nitakuja upesi na nitakuchukua niende nawe. Je,
utakubali?
WAHU. Kwa nini kuniuliza hivyo? Unajua hata ungeniambia hivi
leo ningekubali.
Walianza kufikiria polisi wa Muthaiga. Hakuna motokaa yeyote iliyopita kutoka upande wa mashambani bila kupekuliwa na polisi wa Muthaiga. Askari hawa walikuwa wakali hivi kwamba waliwapiga watu na kuwashitaki kwa makosa madogo kama kuzidisha uzito kwa ratili moja.
Askari wa Thika hawakuogopesha kama askari wa Muthaiga. Hivi sasa, Muthaiga ina tajiri wengi.
Lakini kufika [Kariokor] ilikuwa taabu sana, kwa sababu hakuna mtu aliyekubaliwa na polisi kutembeatembea katika barabara za Nairobi bila pasi. Alikuwako siku ile Mzungu mmoja mkali sana, ambaye aliwashika na kuwatia gerezani Waafrika wote waliokuwa Nairobi bila kazi. Waafrika walimwita “Kifagio”.
Alikata shauri kuingia katika msitu wa Karura na kutembea mpaka afike karibu na Mathare, na hapo angeweza kuvuka mto na kuingia mtaa wa Pangani. Kule angejifananisha na Waafrika wengine waliofanya kazi ya upishi na ayah nyumbani mwa Wahindi.
Hii ndiyo tu biashara Waafrika wangeweza kufanya siku zile. Biashara zingine zote katika mji wa Nairobi zilikuwa zaendeshwa na Wahindi na Wazungu.
Serikali haikuwaruhusu watu kutengeneza pombe. Hata ikiwa ni pombe ya kupeleka mahari wakati wa kuoa, hakuna mtu yeyote angekubaliwa kutengeneza. Yeyote aliyepatikana na kosa hilo, alipelekwa jela au kutozwa faini.
Marejeleo
- Kaburi Bila Msalaba: Hadithi ya Vita vya Mau Mau. 1. Mumbi Ahojiwa. Kareithi, Peter Munuhue. 1969.
- Kaburi Bila Msalaba: Hadithi ya Vita vya Mau Mau. 2. Jani la Maji. Kareithi, Peter Munuhue. 1969.
- Kaburi Bila Msalaba: Hadithi ya Vita vya Mau Mau. 3. Mtaa wa Kariokor. Kareithi, Peter Munuhue. 1969.
- Kaburi Bila Msalaba: Hadithi ya Vita vya Mau Mau. 4. Sherehe ya Kiapo. Kareithi, Peter Munuhue. 1969.
- Kaburi Bila Msalaba: Hadithi ya Vita vya Mau Mau. 5. Mzee wa Lalo Ala Kiapo. Kareithi, Peter Munuhue. 1969.
Mapenzi katika hali ya hatari.