| Random Link ¯\_(ツ)_/¯ | ||
| Aug 29, 2026 | » | Kaburi Bila Msalaba
5 min; updated Sep 5, 2026
Kaburi Bila Msalaba.
Hadithi ya Vita vya Mau Mau.
Kareithi, Peter Munuhue.
1969. Wazungu WeusiWatu kama wewe, wajinga na wasiojiheshimu ni ninyi mnaouza ardhi yetu kwa Wazungu. Ninyi m’Wazungu weusi na ninyi ndio adui wakubwa wa Waafrika. Ni ninyi mnaozuia uhuru wetu. Na ninyi lazima muangamizwe. Askari wake waliomlinda Chifu po pote alipokwenda, walianza kuonyesha hasira walipoona kwamba Mumbi hakumjibu Chifu. Maina, mmoja wao, alianza kushikashika kiboko cha ngozi ya kifaru, alichokichukua kila mahali walipokwenda. Chifu na askari wake walikitumia kiboko hiki kwa kuwapiga wale watu walioshtakiwa kuwa ni wafuasi wa Mau Mau. ... |